25 Machi 2023 - 13:43
Kanaani: Hasira za Netanyahu na Sunak kuhusu mabadiliko ya Asia Magharibi sio jambo ajabu

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuuri ya Kiislamu ya Iran, amejibu matamshi yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu na mwenzake wa Uingereza, Rishi Sunak dhidi ya Iran ya Kiislamu katika mkutano wao hapo jana na kueleza kwamba, si jambo la kushangazwa kutolewa matamshi kama hayo na mawaziri hao.

Nassir Kanaani akizungumzia taarifa za mkutano wa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel na mwenzake wa Uingereza Rishi Sunak ameeleza kuwa, kwa kuzingatia historia mbaya ya tawala hizo mbili na kwa kuzingatia mabadiliko yanayoshuhudiwa hivi sasa katika eneo la Asia Magharibi ambayo ni chanya, hasira na kuchukizwa mawaziri hao na mwenendo huu sio jambo la ajabu.

Kanaani ameongeza kuwa, muelekeo wa mambo hivi sasa katika eneo la Asia Magharibi ni kinyume kabisa na njama za Uingereza na utawala haramu wa Israel ambazo ni kudhoofisha amani na kuleta uharibu katika eneo hili. 

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: Moja ya maigizo ya kudumu ya historia ni utawala haramu wa Israel ambao uwepo wake umetokana na kupora na kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina, unafanya mauaji kila uchao, unamiliki vichwa vya nyuklia na wakati huo huo unakataa kijeuri kabisa kujiunga na Mkataba za Kuzuia Uzalishaji na Usambazaaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).

Aidha amesema, kichekesho kingine cha historia ni pale taifa la Uingereza linapojitokeza na kuituhumu Iran kwamba, eti inateteresha amani na uthabiti wa Asia Maghaaribi katika hali ambayo, sera za utawala waa Uingereza zinashuhudiwa bayana na hazina jingine ghairi ya kuzusha fitina na mifarakano katika maeneo mbalimbali ya Asia Magharibi.

342/